Hasira Hasara - kisa cha nyigu na nyoka na hadithi nyingine
SKU: 70

Hasira Hasara - kisa cha nyigu na nyoka na hadithi nyingine

100 In Stock
7.00€
There is no translation available.

Author: Hassan Adam

Editor: Jörg Berchem

Hadithi hizi za wanyama zilitungwa hapo kale na Aesop (Aisopo), Myunani anayesemekana aliishi Uyunani (siku hizi Ugiriki) mnamo karne ya sita kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hadithi hizi, isipokuwa "Jinsi paka alivyokuja kuishi nasi" na ile ya "Kadhi na masikini" nilizosimuliwa na bibi yangu nilipokuwa mdogo, zimetafsiriwa kwa lugha nyingi ili ziwape wasomaji mafunzo yenye adili. Mimi nimezibadili na, ilipowezekana, nimezipanua kidogo kwa kuziongezea methali ili zionekane za Kiswahili.
Hiki ni kitabu cha pili (cha kwanza kinaitwa "Wimbo wa Bata Bukini na hadithi nyingine za wanyama zenye adili") cha vitabu vichache vya hadithi hizi zenye adili ninavyokusudia, kuvitoa, si kwa ajili ya kuwafurahisha tu, hasa watoto wa shule za msingi, bali viwapatie wasomaji mengi yenye hekima na busara.

  Paperback, 76 pages, illustrations, Kiswahili
Omimee Intercultural Publishers
ISBN-10: 392100814X
ISBN-13: 978-3921008140